Publisher's Synopsis
Pengine swali zuri ni, kwanini usome kitabu hiki?
Jibu rahisi ni kuwa, hiki kitabu ndio mwongozo sahihi kwako kusaka nafasi za chuo na udhamini au ufadhili ughaibuni. Kitabu hiki kinakupa mbinu mahsusi za kufanya maandalizi sahihi na kukuwezesha kupata nafasi ya kujiendeleza ughaibuni. Kwa kuongelea na kuchambua uzoefu wa watu mbalilbali, unajifunza njia sahihi na zenye kuleta matunda mema. Zaidi ya uozefu, kitabu kinakupa namna sahihi ya kupata maelezo zaidi ili ujiandae vyema na mchakato wako wa kusaka ufadhili.Kumbuka, "Kujiandaa kwa ufanisi ni ufunguo wa kupata udhamini!"
Hata kama huhitaji udhamini kwenda kujiendeleza kielimu ughaibuni, kitabu hiki kinakupa mwongozo sahihi wa vitu vya kufanya wakati wa kutuma maombi chuoni na kujiandaa na safari yako.Kitabu hiki kinakuongoza kwenye:
- Kujiandaa vyema wakati wa maombi ya udhamini wa masomo ughaibuni
- Kwa maelezo mahsusi yanayoainisha utafutaji wa vyuo na ufadhili ughaibuni.
- Kinakusaidia kuandaa nyaraka muhimu kwa wakati, ikiwemo vyeti, cv, barua za mapendekezo (recommendation letters) n.k.
- Maelezo ya udhamini kulingana na nchi
- Kinachambua fursa muhimu za udhamini wa masomo kwa kila nchi.
- Kinakupa muda mwafaka wa kuomba kila udhamini ughaibuni
- Ushauri juu ya kuchagua sehemu sahihi ya kwenda kujiendeleza
- Uchambuzi wa nchi na faida kwa kila udhamini utolewao
- Mbinu za kujipanga ili kufaidika baada ya kuhitimu safari ya kielimu.
- Maandalizi muhimu kabla ya safari
- Kujiandaa kwa safari ya masomo ughaibuni (visa, makazi, mazingira ya kielimu).
- Mwongozo wa kukabiliana na mazingira mapya, tamaduni mpya na mifumo ya elimu ya kimataifa.
Kitabu hiki kimeandaliwa na WaUKAYA:
- NOEL MZUNGU,
- GODFREY KIMATHY,
- COLIN MTITA.